Na Mwandishi wetu
Kikundi cha Sauti ya jamii kipunguni Leo imetoa mafunzo kwa mafundi vyereani wa mtaani 40 ili kuweza kushona barakoa kwa muongozo wa wizara ya afya pamoja na vitakasa mikono.
Akifungua mafunzo hayo yalioandaliwa na kikundi hicho kwa ufadhili wa women Fund kupitia mradi wa zuia ukatili, wezesha wanawake na watoto kupambana na Covid-19 kwa ustawi wa jamii,afisa Maendeleo wa kata ya Kipunguni Betty Mzava amewataka wanawake hao kuweka umakini katika mafunzo wanayopatiwa na Kikundi hicho ili matunda yaweze kupatikana.
Amesema kuwa Kikundi hicho kimeweza kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia katika kata hiyo pamoja na kata jirani kutokana na harakati wanazozifaya.
Aidha amewataka wanawake hao kumuunga mkono Rais John Magufuli kwa kufuata maelekezo aliyoyatoa kwa kutambua Corona ipo lakini watu waendelee kujinga na kufanya kazi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa kikundi hicho Seleman Bishagaz amesema kuwa, mradi huo ni wa miezi miwili ukijumuisha ushonaji wa barakoa pamoja na utengenezaji wa vitakasa mikono.
Ameongeza kuwa, pia kutakuwepo na mafunzo ya uwelewa wa masuala ya haki za wanawake na wasichana kwa washiriki 60, madhara ya rushwa ya ngono pamoja na kuibua visa vya ukatili vilivyojitokeza kipindi cha ugonjwa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona.
Amesema kuwa, lengo la mafunzo hayo ni kutokomeza ugonjwa wa Corona, kuwapa njia za kupata kipato mbadala wanawake na wasichana ambavyo vimeathirika kwa ugonjwa huo pamoja kuizuia garama za kupata vifaa kinga vya Covid 19 .
Nae Amina Shifta mkaazi wa kipunguni ambae ni miongoni mwa wanawake waliopatiwa mafunzo hayo amesema ataweza kutengeneza vitakasa mikono na kushona barakoa zenye viwango vinavyohitajika.
"Mwanzo nilikua nashona tu barakoa wala kutengeza vitakasa mikono nilikua sijui Ila kupitia mafunzo haya nitaweza hata kuwafundisha na watu wengine maana nimejifunza kwa weledi"amesema Amina
0 Comments