Mkuu wa mkoa wa Kusini Unguja, Ayoub Mohammed Mahmoud amejitokeza kuchukua Fomu ya Kuwania nafasi ya Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM.
Ayoub anakuwa mgombea wa 23 kufika katika ofisi kuu za Chama hicho zilizopo Kisiwandui Mjini Unguja na kukabidhiwa fomu na katibu wa kamati maalumu ya NEC,Idara ya organization Zanzibar Cassian Galos Nyimbo.
Mara baada ya kukabidhiwa Fomu Ayoub aliwaambia waandishi wa habari kwamba hana mengi ya kuzungumza kwa siku ya leo hivyo anaomba wamuombee kwa mchakato aliuanza.
“Najua ndugu zangu wana habari munahamu ya kutaka kunisikiliza, lakini niwaombe radhi kuwa sitokuwa na mengi kikubwa naomba muniombee kwa mungu” alisema Ayoub.
Hadi sasa Jumla ya wagombea 23 tayari wameshajitokeza Ofisini hapo kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama cha Mapinduzi Zanzibar ambapo kwa Siku ya leo wagombea wanane waliojitokeza.
0 Comments