Na Zakayo Chelesi
Idara ya vyuo na vyuo vikuu Uvccm Mkoa wa Njombe imejitokeza
kumdhamini mwenyekiti wa Ccm taifa ambaye pia ndiye Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Magufuli huku ikieleza kuwa wamejipanga kuleta ushindi
wa kishindo katika uchaguzi mkuu kwa mwaka 2020-2025.
Akizungumza Mwenyekiti wa Idara hiyo Seleman Matembwi
amesema kuwa wao kama vijana wa vyuo ndani ya umoja wa vijana Uvccm mkoa wa
Njombe wameamua kumdhamini Rais Magufuli kwa sababu ya juhudi zake alizo zioenyesha
katika kipindi cha miaka mitano kwa mafanikio makubwa aliyoyafanya nchini Tanzania.
Sambamba na hayo Mjumbe wa idara hiyo mkoa wa Njombe Chrispin Kalinga ameongeza kwa kusema kuwa wao
kama vijana wa mkoa wa Njombe wamejipanga vizuri kuelekea uchaguzi mkuu wa
mwaka 2020-2025 kuhakikisha wanakipatia ushindi wa kishindo wa chama cha
mapinduzi Ccm katika ngazi za madiwani,Wabunge na Rais.
Mjumbe huyo aliongeza kwa kuwataka vijana wa mkoa wa njombe
kuhakikisha wamejipanga kikamilifu kuona namna wanavyo weza kukisaidia chama
kupata ushindi katika uchaguzi mkuu kwenye maeneo yao.
Katika hatua nyingine Mwakalinga akaongeza kwa kuwaomba vijana
wajitokeze kuwanania nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo udiwani na ubunge
kwenye maeneo yanayo wazunguka akiamini vijana wanaweza.
“Naomba nitumie nafasi hii kuwaomba vijana wenzangu msisite
kujitokeza pindi taarifa za kuanza kujaza fomu mkoani kwetu itakapo tangazwa
rasmi mjitokeze mkachukue na kujaza nafasi mbalimbali haswa ya Udiwani na
ubunge naamini vijana ni nguvu kazi ya taifa na tunaweza kikubwa ni ku jiamini na
kudhubutu kwasababu sisi ni nguvu kazi ya leo na ni chachu ya maendeleo ya Njombe na taifa kwa ujumla.”aliyasema
Mwakalinga.
Pia baadhi ya wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali ikiwemo chuo
cha Amani na chuo cha Ekros sabasaba walio jitokeza kumdhamini Rais Magufuli wamongea
kwa kusema kuwa wao hawajalazimshwa na mtu bali ni kwa hiyali yao kumdhamini
kiongozi huyo kwasababu ya mambo makubwa aliyo yafanya katika msimu unao isha.
Wakamaliza kwa kusema kuwa wao kama wanafunzi wa idara ya
vyuo na vyuo vikuu Ccm wamejipanga kikamilifu kuhakikisha wanafanya mageuzi
katika mkoa wa njombe kwa kuhakikisha kila kata za mkoa wa Njombe pamoja na
majimbo yote yaliyomo kwenye mkoa huo chama cha mapinduzi kinatawala.
0 Comments