TANGAZA NASI

header ads

ACT Wazalendo wafungua pazia la uchukuaji fomu za Urais,diwani na Ubunge






Kamati Kuu ya Chama cha ACT Wazalendo,imefungua rasmi pazia la mchakato wa uteuzi wa wagombea wa Uchaguzi mkuu 2020. imesema zoezi la kuchukua,kujaza na kurejesha fomu za Udiwani,Ubunge na Urais litafanyika kuanzia Julai 01,2020 hadi Julai 13,2020.

Katibu mkuu wa Chama hicho Ado Shaibu amesema

Kuchukua na kurejesha fomu za ugombea wa Udiwani, Uwakilishi, Ubunge na Urais. Kamati Kuu imefungua rasmi pazia la mchakato wa uteuzi wa wagombea wa Uchaguzi Mkuu 2020. 

Amesema 

Zoezi la kuchukua, kujaza na kurejesha fomu litafanyika kuanzia tarehe 01 Julai 2020 hadi tarehe 13 Julai 2020 Hivyo basi, ninapenda kuchukua fursa hii kuwatangazia wanachama wote wa ACT Wazalendo wenye nia ya kugombea kwenye nafasi za Udiwani, Ubunge, Uwakilishi na Urais wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakachukue fomu ifikapo tarehe 01 Julai 2020 hadi 13 Julai 2020.

"ACT Wazalendo haitamvumilia mwanachama yeyote atakayejihusisha na vitendo vya rushwa kwenye zoezi la uteuzi wa wagombea wake."
Katibu mkuu wa chama


Post a Comment

0 Comments