PIERRE Emerick Aubameyang, mshambuliaji wa Arsenal amepewa onyo la kufikiria kutaka kuondoka ndani ya Klabu hiyo inayompa nafasi kwani akifanya hivyo atapotea kwenye ramani ya soka.
Ian Edward Wright, mshambuliaji wa zamani wa Arsenal ambaye alicheza msimu wa 1991-98 akicheza jumla ya mechi 221 na kutupia mabao 128 amesema kuwa akiendelea kuwasumbua Arsenal atapotea.
Nyota huyo amesema kuwa anatambua malengo ya Aubameyang ni kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ila ili kufikia hayo ni lazima awe na subira kwani nafasi yake ya kufanikiwa ndani ya Arsenal ni kubwa.
"Mkataba ambao anapewa na Arsenal ni mkubwa na anapaswa auheshimu akisema alete jeuri anaweza kushangaa anaanza kuchezea benchi labda Kocha Mkuu, Mikel Arteta anaweza kumpa nafasi (Gabriel) Martinelli, yeye atafunga lini?
0 Comments