MBUNGE wa Iringa mjini (CHADEMA) Peter Msigwa, leo Juni 14, 2020 ametangaza nia ya kugombea Urais kwa tiketi ya chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 2020. Vile vile Msigwa amesema endapo Chadema kitampitisha mgombea mwingine atarejea kutetea tena nafasi za jimbo lake "Ikiwa chama changu kitanipitisha niwe mgombea wa Urais,Ubunge sitagombea tena kwenye jimbo langu,lakini chama changu kisiponipitisha kikamteua mwingine,mimi nitaungana na huyo aliyeteuliwa na chama changu kumpigia debe lakini nitagombea jimbo langu la Iringa Mjini"
0 Comments