Na Amiri kilagalila,Njombe
Watu 13 wamenusurika kifo baada ya basi la abiri
lenye namba za usajili T 802 DEZ kampuni ya Dosmeza linalofanya safari zake
Njombe-Iringa kuacha njia na kutumbukia mto Ichunilo June 11,2020 majira ya saa
moja na dakika hamsini,baada ya kumaliza mteremko mkali wa Ruhuji mjini Njombe.
Akizungumza mara baada ya kupokea majeruhi wa
ajali,Mganga mfawidhi wa hospitali ya mji wa Njombe (Kibena) Dkt,Alto Damas
Mtega,amesema walipokea majeruhi 13 na kuwapa huduma ya kwanza.
“Tulifanikiwa kuwapokea majeruhi wote na kuwapa
hduma ya kwanza na kuwapa matibabu na majeruhi 3 tuliwaruhusu usiku ule ule
kwasababu hali zao hazikuwa mbaya,majeruhi wengine 10 tunao wodini bado
wanaendelea na huduma za matibabu,katika hao mmoja hali yake sio nzuri lakini
matarajio yetu ataendelea kuwa vizuri”alisema Alto Mtega
Nuhu George na Kissa Mwaisongole,ni majeruhi katika
ajali hiyo wanasema walitembea salama
kutoka Iringa na dereva wa gali hiyo alikuwa ni mwaminifu lakini tatizo ni
kufeli breki katika mteremko huo.
“Dereva wetu alikuwa mwaminifu na alijitahidi ili
kuokoa roho zetu na tulitembea salama mpaka kufika hapa gari ikakosa breki
ikaluka na ikaingia kwenye maji”alisema Kissa Mwaisongole
Aidha kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa
amesema basi hilo limepata ajali katika mteremko mkali kutokana na kushindwa
kukata kona kwasababu ya mwendo kasi.
“Basi hili halikuweza kukata kona kama ilivyo ina
maana limekuja na mwendo ambao ni kasi,sasa kitakachofanyika hapa ni kuchunguza
kama wakati linashuka lilikuwa mwendokasi ama kuangalia Mechanical diffect,na
uchunguzi utakapokamilika sheria itafuata mkondo wake”alisema Hamis Issa
Hata hivyo kamanda ametoa wito kwa madereva wote
kuchukuwa tahadhari kubwa wanapoingia mji wa Njombe mara baada ya kufika katika
mteremko huo.
“Enyi madereva wengine kutoka mikoa mingine,hali ya
barabara mkoa wa Njombe ni milima na kona kali chukueni tahadhar mnaopo kuja
huku hakikisheni magari yana breki za kutosha na muendeshe kwa tahadhari kubwa
tuepukane na madhara kama haya yanayotokea”aliongeza kamanda.
0 Comments