TANGAZA NASI

header ads

Naibu waziri Bashe akutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkazi wa shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP)



Naibu Waziri Kilimo Mhe.Hussein Bashe leo amekutana na Mkurugenzi Mkazi  wa shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Bw.Michael Dunford Ofsini kwake ambapo walifanya mazungumzo mafupi.

Wakiwa katika kikao hicho kifupi Bw.Michael amesema ujio wake umelenga kuagana na uongozi  wa wizara kwa niaba ya wafanyakazi wote  kwa kuwa amepangiwa kazi nyingine  ya kuwa Mwakilishi wa WFP katika nchi za Afrika mashariki ambapo makao makuu  yake yapo jijini Nairobi Nchini Kenya.

Bw. michael ameleza kufurahishwa na utendaji kazi wa serikali kupitia wizara ya kilimo ambapo miradi mingi chini ya WFP ilitekelezwa kwa ufanisi mkubwa.

Pia amemshukuru Mhe.Bashe kwa namna wizara walivyoweza  kushirikiana naye wakati wa uongizi wake ambapo amekiri kwamba ushirikiano huo ulisababisha kutekeleza majukimu yake kwa ufanisi zaidi  alisema Bw.Michael.

Naye Naibu Waziri Kilimo Mhe. Bashe mara baada ya shukrani hizo amemuomba Bw. michael kufikisha ujumbe Wfp kwamba  waongeze wigo wa  ununuzi wa mazao ya kilimo nchini hapa yakiwemo mtama na  ngano badala ya mahindi peke yake ili wakulima waweze kupata fursa nyingine  ya soko la mazao hayo.
"Tumekuwa tukifanya biashra na WFP hasa ya mazao ya mahindi kwa muda sasa kupitia wakala wa uhifadhi wa Chakula nchini NFRA jambo ambalo limesaidia kuongeza soko na ubora wa mahindi kwa wakulima lakini tunadhani sasa muongeze wigo katika kununua mazao mengine kama ngano na mtama  kwakuwa mahitaji yake ni makubwa,, alisema Mhe. Bashe.

Aidha Mhe.Bashe alimalizia kwa kusema  kwamba Wizara ya Kilimo itaendelea kushirikiana na Shirika hili kwa kuwa wamekuwa wadau wakubwa katika kushughulikia masuala muhimu ya usalama wa Chakula na lishe katika taifa letu.

Post a Comment

0 Comments