TANGAZA NASI

header ads

CCM wampongeza Rais Magufuli


Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu Taifa CCM katika kikao chake leo Dodoma ikiongozwa na Dkt. Magufuli, Rais wa Tanzania na Mwenyekiti CCM Taifa, imeridhishwa na maandalizi ya uchaguzi mkuu na kuelekeza kutolewa kwa ratiba ya mchakato wa ndani wa uteuzi wa wanaoomba dhamana ya uongozi katika vyombo vya Dola.

“Kamati Kuu imepokea taarifa ya maendeleo ya uandishi wa mweleko wa Sera za CCM kwa mwaka 2020-2030 na kujiridhisha kuwa kazi nzuri imefanyika mpaka ngazi ya rasimu ya pili, imepitia kwa mara ya pili taarifa ya uandishi wa Ilani ya CCM katika uchaguzi mkuu wa 2020”-POLEPOLE

“Kamati Kuu imepokea taarifa ya Serikali juu ya mapambano ya dhidi ya corona na hatua ambazo zimechukuliwa kuukabili ugonjwa huo kwa mafanikio Tanzania, na kwa kauli moja kikao kimempongeza Rais Magufuli kwa msimamo thabiti usioyumba katika kipindi chote cha corona”-POLEPOLE

Post a Comment

0 Comments