Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas anafanya ziara leo nchini Israel, kumuonya waziri mkuu wa nchi hiyo Benjamin Netanyahu dhidi ya mpango wa kuyanyakua maeneo ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi.
Kuyanyakuwa kwa nguvu maeneo ya Ukingo wa Magharibi yenye makaazi ya walowezi wa kiyahudi, ni sehemu ya mpango wa amani wenye utata uliotangazwa na rais wa Marekani Donald Trump.
Waziri Maas anatarajiwa kuieleza Israel kuwa Umoja wa Ulaya unapinga vikali unyakuzi huo, na kwamba Ujerumani ambayo itakuwa mwenyekiti wa Umoja wa Ulaya kuanzia Julai mosi, inaweza kuwa na kauli nzito katika uwezekano wa kuiwekea vikwazo Israel kuhusiana na mpango wake huo.
0 Comments