“Mimi nina miaka 50 kasoro miaka 3, nimefanya mengi,
Kiwanda cha Muziki kimenipa mengi, Watoto wangu wanasoma chuo Nje ya nchi wa
kwanza na wapili, hivyo mafanikio nimeshapata, ni muda sasa kwenda kuwatumikia
Raia wa Rombo kwa kuwa Mbunge wao”-
(via XXL ya Clouds FM)
“Sijawahi kuisaidia jamii yangu ya Watu wa Rombo,
Mungu amenijaalia uwezo kiasi hivyo nafahamu matatizo yanayoikumba Rombo na
ningependa kuwasaidia, hivyo hilo ndio jambo linalonisukuma zaidi”-
(via XXL ya Clouds FM)
"Mimi nipo CCM tangu zamani, natangaza nia,
uchaguzi wa mwaka huu, Chama kikinipa nafasi nitagombea Rombo, Kilimanjaro kule
ndio kwetu, Mbunge wa sasa kule ni Mzee wetu Selasini, naenda Rombo ili
kuwatumikia Wananchi” -
(via XXL ya Clouds FM)
“Kuhusu kufunga ndoa na Shaa tumekamilisha mipango,
mwaka huu lolote linaweza kutokea, kwa kuwa nimetangaza nia ya kugombea Ubunge
kule Rombo, Kilimanjaro mwaka huu, najua ukiingia kwenye siasa moja ya silaha
wataitumia ni hiyo hajaoa anaishi na hawara”-
(via XXL)
0 Comments