TANGAZA NASI

header ads

Livingstone Rangers Fc yaahidi kurudi na ushindi kutoka Ruvuma.


 Na Zakayo Chelesi
Katibu wa timu ya mpira wa miguu Livingstone Rangeras Fc ya Mkoa wa Njombe ndg Wilfred Willa amewaambia waandishi wa habari kuwa timu hiyo
tayali ipo mkoani ruvuma na tayali imejipanga kwaajili kuanza mchezo wao utakao chezwa katika uwanja wa Ccm Tunduru na katika mchezo huo wa tarehe 27 jun2020 watachuana vikali na timu ya Lindi United..

Katika hatua nyingine kiongozi huyo aliongeza kwa kusema kuwa timu hiyo inayo wakilisha mkoa wa Njombe ipo tayali kupambana na kuleta ushindi ndani ya mkoa wa Njombe na hatimaye kuingia Ligi daraja la pili kama ilivyo dhamira ya timu hiyo kuleta matumaini kwa wananjombe kwa kuongeza timu ziwe nyingi na zenye viwango ndani ya mkoa wa njombe.

"Naomba nisema kwamba ndg waandishi wa habari timu ya Livingstone ni timu ambayo imeanza miaka hivi usoni hivyo hata kufika hatua hii tunapaswa kumshukuru Mungu,lakini pia nisiwasahau wananchi wa mkoa wa Njombe kwakuendelea kuipenda na kuichangia timu hii maana bila wao tusingekuwa katika hatua hii hivyo tunakwenda Ruvuma ninauhakika tunarudi na ushindi"aliyasema Willa.

Sambamba na hayo kiongozi huyo mwandamizi aliongeza kwa kusema kuwa timu hiyo inategemea michango kutoka kwa wananchi na akaongeza kwa kusema kuwa,"Nitumie nafasi hii  kuwaomba watanzania wote mchango wao kwa hali na mali ili kufanikisha mambo mbalimbali ya mahitaji ya Kambi kama vile chakula,sabuni na posho za wachezaji,yote hiyo tunaomba kutoka kwenu wananchi wa Njombe kutuchangia chochote utakacho guswa".

Hali kadhalika akaongeza kwa kusema kuwa anaomba mchango wowote na mchango huo utumwe kwenye sim namba zifuatazo,0757051440 au 0757592824.

Kwa upande wake Afisa habari wa timu hiyo ndg Chrispin Kalinga amesema kuwa hana wasiwasi na kikosi chake mahili kilicho sukwa chini ya kocha Mwandamizi Hassani Rashidi anaamini kwa usajili ulio fanyika anakwenda kuleta ushindi mkoani Njombe.

Akamaliza kwa kusema kuwa anawaomba wananchi wa njombe kuendelea kujitolea kuichangia timu hiyo ili ipate mafanikio na kurudisha matundanda mazuri ndani ya mkoa wa njombe. 

Post a Comment

0 Comments