Mahakama ya Hakimu Mkazi Njombe imemtia hatiani na kumhukumu kulipa faini ya Shilingi Milioni 5 au kifungo Cha Mwaka mmoja jela Mwandishi wa habari Prosper Mfugale baada ya mwandishi huyo kukiri kutoa maudhui Katika Mtandao wa YouTube  bila ya kuwa na leseni kutoka mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA), hata hivyo Mfugale amelipa faini hiyo na kuachiwa huru.

Mfugale alikamatwa mnamo Februari 29 Mwaka huu na kushikiliwa kwa siku nne kituo cha polisi Njombe na tarehe 4 Machi alifunguliwa mashitaka ya kutoa maudhui mtandaoni bila ya kuwa na leseni kutoka Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kinyume cha Sheria ya Maudhui Mtandaoni ya mwaka 2018.
Wakili Chance Luoga kutoka mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania alikuwa anasimamia Kesi yake tangu alipokamatwa.
(Watetezi TV)