DODOMA
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (kazi,ajira na vijana) Mh Antony Mavunde amewata wakazi wa kata ya nzinje mkoani Dodoma kutumia fedha za fidia walizolipwa na shirika la maendeleo ya Petrol Tanzania kuboresha maisha yao kwa kujenga vitega uchumi vitakavyowasaidia kuwaletea maendeleo katika eneo hilo.
Mh mavunde ametoa wito huo katika kata hiyo wakati wa zoezi la ulipwaji wa fidia wa zaidi ya shilingi milioni mia moja na ishirini kwa wakazi 19 wa kata hiyo uliowahusisha wananchi hao pamoja na shirika la maendeleo ya petrol na kusema kuwa wananchi hao wanaweza kubadili maisha yao kwa kuhakikisha wanatumia vizuri fedha hizo na kuliboresha eneo kutokana na kuliendeleza eneo hilo .
Katika hatua nyingine amewasihi wakazi wa kata hiyo kuwapa ushirikiano wawekezaji hao kwa kuwa wamedhamiria kuwaletea maendeleo wakazi hao na kwamba anayo dhamira ya dhati katika kuboresha maisha ya wakazi wa eneo hilo ikiwa ni pamoja na kuwapatia ajira vijana wanaozunguka eneo hilo la mradi.
Naye mkurugenzi mkuu wa shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC) Bwana James Mataragio amesema shirika lake linatekeleza sera ya nchi ya Mh Rais Dr John Magufuli ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati kwa kuboreshja mazingira kwa kujenga viwanda katika maeneo mbalimbali hapa nchini na hivyo kuwaletea wananchi maendeleo.
Kwa upande wake mtendaji wa kata ya zuzu bwana mabrouk sefu amelishukuru shiriki la TPDC
kuwalipa wananchi hao fidia kwa wakati na amewaomba wananchi hao waliolipwa fidia kutoitumia ardhi hiyo kwa shughuli nyingine yoyote kuwa tayari shirika limeonyesha kuwajali na kuwathamini wananchi hao waliotoa eneo hilo kwa ajili ya uwekezaji huo
Hatahivyo ,lengo la shirika la maendeleo ya petrol tanzania (TPDC) ni kuhakikisha wanafikisha huduma karibu na wananchi na hivyo kuwezesha urahisi wa kupatikana kwa bidhaa ya mafuta karibu na wananchi na kuwapunguzia gharama ambazo zinaweza kuepukika
0 Comments