Aliyekuwa mbunge wa Arusha
Mjini (Chadema), Godbless Lema, amesema kukosekana uelewa wameshusha thamani ya
Tanzanite kwa hali ya juu.
“Piece ya kilo 9.27 na 5.28 ni
unique pieces ambazo kwa bei mnayo pigia kelele sio zaidi ya USD 3.5 milioni,”
aliandika Lema katika ukurasa wake wa twitter.
“Najiuliza sasa ni pieces
gani nyingine zitapata thamani kuonyesha upekee wa madini haya,” aliandika
Lema.
Lema amesema madini
hayo ambayo ni adimu bei zake hazipangwi kwa gramu isipokuwa upekee.
“Kuna rules katika biashara
hizi, rules hizo hazihitaji degree/PHD isipokuwa wall street thinking. Nani
ataona thamani ya Tanzanite kwa kilo 9.27/5.28 kuuzwa sawa na saa ya Mike Tyson
na mnunuzi ni serikali?,” aliandika Lema Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kwa kukosa uelewa mmeshusha thamani ya Tanzanite kwa hali ya juu sana, piece ya
kilo 9.27 na 5.28 ni unique pieces ambazo kwa bei mnayo pigia kelele sio zaidi
ya USD 3.5 milioni.Najiuliza sasa ni pieces gani nyingine zitapata
thamani kuonyesha upekee wa madini haya ?
0 Comments