"Hili suala la madereva ambao mmeona clip inatembea ikionesha Mabasi ya Rungwe na Happy Nation wanakimbizana ili kuona nani wa kwanza kufika kwenye stendi fulani, tumekuja kubaini hawa madereva wali-bet hiki kitendo tunakikemea kwa nguvu"- Kamanda Musilimu.

"Sheria inanipa uwezo wa kuwaondolea sifa wa kuendesha haya magari ya mizigo na biashara na kwa miezi 6, hawa hawatokuwa barabarani wakiendesha magari labda hivi vigari vidogo"- Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Fortunatus Muslimu.