DODOMA
Shirila la Raleigh Tanzania linaendelea na
Kampeni yake ya Uwajibikaji wa Jamii Kupitia Vijana yenye lengo la kuhamasisha
jamii nyingi kuona umuhimu wa kufanya ufuatiliaji wa miradi na huduma
zinazotolewa.
Mradi huo unatumia Mfumo wa kujenga jamii adilifu
ambao unashirikisha wananchi wenyewe kutafuta suluhisho la changamoto
zinazojitokeza kwenye miradi au huduma katika jamii.
Akizungumza kwa njia ya simu na kituo hiki kuhusiana
na jamii yenye uadilifu, Mratibu wa kampeni hiyo kutoka wilayani Chamwino
William Luhunde amesema kuwa jamii yenye uadilifu ni mfumo ambao umewekwa
kwaajili ya kuongeza uwajibikaji na uwazi katika utekelezaji wa miradi.
‘’Lakini katika mfumo huu ni mfumo unao wezesha
makundi maalumu kama wanawake ,vijana na watu wanaoishi na ulemavu lengo kuu ni
kuwafanya washiriki katika kutoa maoni yao kuhusu miradi’’ Wiliam
Kuruthumu Ayubu yeye ni mfuatiliaji wa miradi ya
jamii katika kampeni hiyo kutoka wilayani chemba kijiji cha Mtoro Mkoani hapa
amesema kuwa wanakijiji wa kijiji hicho wamekuwa wakiwajibika ipasavyo kwani
mradi huo wameweza kuupokea vizuri .
‘’Wameupokea mradi huu vizuri wanautunza hawauharibu
na wanajua kabisa unafaida ndio maana wanatunza na wawajibika kuutunza sio
mmoja ni wote wanaume,wanawake,watoto hasa vijana’’Kuluthumu
Akizungumzia maendeleo ya vijana katika mradi na
nini kifanyike, Mratibu wa kampeni Dodoma Mjini Halima Seleman amesema kuwa
vijana wanamchango mkubwa wa kuhakikisha kuwa miradi waliyonayo inakuwa na
mafuaa katika jamii .
‘’kuna vijana ambao ni wafuatiliaji wako katika
vijiji na mitaa mbalimbali ambayo tunafanya kazi au tunatekeleza mradi huu
,kwanza kabisa vijana tunatakiwa kupewa elimu ya umuhimu wa sisi kushiriki
katika miradi mbalimbali ya maendeleo tupewa kipaumbele pale yanapokuja masuala
ya kimaendeleo katika jamii yetu kwasababu tunaamini kwamba vijana ndio nguvu
kazi ya Taifa’’ Halima
Lengo la kampeni hiyo ni Kuhamasisha jamii kufanya
ufuatiliaji wa miradi na huduma katika maeneo yao na kuwa wawajibikaji lakini
pia Kuhamasisha wananchi kupata taarifa kuhusu miradi na umuhimu wa kushiriki
kwenye pamoja na Kufahamu umuhimu wa Uwajibikaji katika jamii na kuunda Kikundi
kazi ili kutatua changamoto.
Raleigh Tanzania ni shirika lisilo la kiserikali
linalofanya kazi katika kusaidia miradi ya maendeleo endelevu na imejikita
katika kufanya kazi kwa kushirikiana na vijana kwa kuwahamasisha kuleta
maendeleo chanja katika maeneo makuu ambayo ni kujenga jamii isiyo tegemezi
(Community Resilience),Maji na usafi wa mazingira (water anda sanitation na
kuwawezesha vijana katika ujuzi na uwezo wa uongozi (Youth Leadership)


0 Comments