TANGAZA NASI

header ads

Halmashauri ya mji Kondoa yakusanya zaidi ya sh billion 1.3, yawa ya kwanza katika halmashauri za miji Tanzania


Wilaya ya halmashauri ya mji Kondoa chini ya mkurugenzi wake msoleni dakawa  imeeleza mafanikio makubwa waliyoyapata katika ukusanyaji wa mapato ya ndani,kihistoria katika mwaka wa fedha 2016 – 2017 baada ya halmashauri kuanzishwa bajeti ilikuwa million 16, lakini bajeti ya fedha ya mwaka 2018 – 2019 bajeti ilipanda mpaka kufikia million 840.

 Mwaka wa fedha 2018 – 2019 bajeti ilikuwa million 837.526 kwa mwaka huu wa fedha halmashauri  ilikusanya billion 1.129 ambayo ni sawa na asilimia135% ya lengo la bajeti na mpaka ikapelekea halmashauri ya mji Kondoa kuwa halmashauri ya kwanza katika halmashauri za miji Tanzania katika ukusanyaji mapato.

Pia kwa mwaka huu wa fedha wa fedha 2019 – 2020 halmashari iliweza kudouble bajeti mara mbili kutoka million 837.526 mpaka kufikia billion 1.6 ambayo mpaka kufikia mwezi wa 5 tarehe 31  halmashauri ya mji Kondoa imekusanya jumla ya zaidi ya sh billion 1.3 ambayo ni sawa na asilimia 80 ya lengo.

Post a Comment

0 Comments