DODOMA
Shirila lisilo la
kiserikali la Wanawake Amkeni ‘Women Wake Up (WOWAP) limeendelea kuunga mkono
juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa corona .
Shirika hilo limeanza
kutekeleza mradi mwingine wa COVID 19 katika Halmashauri ya wilaya ya Chamwino
lengo lake likiwa ni kufanya hamasa ya kuweza kuhakikisha kuwa wanawake
na watoto wanakuwa sehemu ya kujikinga na maambukizi ya maradhi hayo kwa kupata
uelewa wa namna gani maradhi hayo yanaenezwa na kuchukua juhudi za makusudi
katika kujikinga .
Mratibu wa wa shirika
hilo Nasra Suleiman amesema kuwa wamelenga wanawake na watoto kwasababu wako
katika eneo hatarishi huku akibainisha kuwa wanawake wamekuwa wakijichanganya
katika shughuli mbalimbali za kijamii .
Amesema katika mradi
huo wanatumia watalaamu wa Afya ambao wana ubobezi katika masuala ya Afya ya
kuona ni namna gani wanaweza kutoa elimu ya kuhakikisha kuwa wananchi wanaelewa
kuhusu ugonjwa corona.
Kwa upande wake Asha
Msengwa Afisa Afya wa Halmashauri ya Wilaya ya chamwino lakini pia ni
mwenyekiti kamati ya kamati ya kusimamia masuala ya COVID-19 wilayani humo
amesema wanamikakati mbalimbali katika kuendelea kuhamasisha jamii katika
masuala mbalimbali ya kiafaya na ya kijamii kwa ujumla.
Hatahivyo amesema kuwa
wataendelea kutoka elimu na kuhakisha kwamba wanafuata miongozo yote ambayo
imekuwa ikitolewa na wizara ya Afya.
0 Comments