Chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Njombe kupitia kwa katibu wa Siasa na uenezi mkoa Ndug,Erasto Ngole kimetangaza kumfutia uanachama yeyote atakayepinga maamuzi ya vikao hasa vya uteuzi wa wagombea.
Ngole ameyasema hayo mkoani Njombe wakati akifanya mahojiani na kituo cha Radio King's kilichopo mjini Njombe.
"Kwenye mchakato wa Uchaguzi tunaouendea sasa Ikitokea Mwanachama anapinga maamuzi ya vikao hasa uteuzi wa Wagombea kuwa kwanini huyu ameteuliwa kupeperusha Bendera ya Chama kugombea nafasi fulani huyo atafutwa uanachama maana si mwenzetu" Erasto Ngole Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Mkoa wa Njombe.
(Via:King's Redio)
Sambamba na hilo Ngole amezungumza mambo yanayohusu Chama na mchakato wa uchaguzi yakiwemo.
"Wanachama wetu wa CCM wenye nia ya kugombea nafasi za uongozi waendelea kuwa watulivu hadi hapo Chama kitakapotoa Maelekezo ya kuanza rasmi mchakato"Erasto Ngole Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Mkoa wa Njombe.
(Via:King's Redio)
"Muda ukifika kila mmoja ana haki ya kugombea Nafasi yeyote bila kutishwa na Mtu yeyote kwakuwa hiyo ni haki yake kwa mujibu wa Katiba ya Chama kikubwa Wanachama wazingatie Kanuni za Mchakato" Erasto Ngole, akizungumza na King's Redio Njombe
"Wapo baadhi ya viongozi wa Kata na Majimbo wamekuwa wakisema hii Kata yangu au Jimbo langu Chama tunasema hakuna Kata wala Jimbo la mtu mmoja bali ni Wananchi ndio maana hiyo nafasi ulipewa na wengi ili uwawakilishe" Erasto Ngole Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Mkoa wa Njombe.
(Via:King's Redio)
"Muda wowote tutakapo pokea Maelekezo toka Chama ngazi ya Taifa pamoja na vikao vyetu nitakuja kwenye Vyombo vya Habari kuwajulisha ninyi Waandishi na Wanachama kuwa sasa Mchakato umeruhusiwa Rasmi ili kila mmoja aende akawanie nafasi husika" Erasto Ngole Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Mkoa wa Njombe.
(Via:King's Redio)
"Muda ukifika Diwani au Mbunge atakaetetea nafasi yake atakuwa Mgombea kama Wagombea wengine hivyo atapaswa kuzingatia Kanuni za Chama kwakuwa Ile nafasi ya awali itakuwa imekoma hadi hapo Wanachama watakapo mchagua yeye au Mwingine watakaeona anafaa kwa wakati husika"Erasto Ngole Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Mkoa wa Njombe.
(Via:King's Redio)
"Kwenye Mkoa wetu hatutavumilia uzembe ambao utafanywa na Vikao vya ngazi husika zikiwemo Kamati za Siasa za Kata na Wilaya endapo tutapata Malalamiko yenye Uhakika kuwa Kamati hizi zimekiuka Kanuni tutaziwajibisha kabla sisi Mkoa hatujawajibishwa na Taifa" Erasto Ngole Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Mkoa wa Njombe.
(Via:King's Redio)
"Tumeshaelekeza Muda ukifika hakuna Diwani Wala Mbunge atakaekuwa juu ya maamuzi ya Wanachama tukibaini hilo atashughulikiwa kama Wagombea wengine maana akiachwa atahatarisha usalama wa Chama Chetu" Erasto Ngole.Erasto Ngole Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Mkoa wa Njombe.
(Via:King's Redio)
"Chama kwenye Mkoa kupitia Viongozi na Vikao husika tumejipanga na tumeanza kuwashughulikia wale ambao wameanza Kampeni kabla ya Wakati wote tumeanza kuwabaini hao wajitafakari" Erasto Ngole, Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Mkoa wa Njombe.
0 Comments