Na Omary Mngindo, Chalinze
UONGOZI wa Halmashauri ya Chalinze, wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, chini ya Kaimu Mkurugenzi Zainab Makwinya, imewatembelea Wajasiriamali wadogo kwa lengo la kuwahamasisha kununua vitambulisho vya biashara.
Makwinya akiambatana na ofisa Tehama Sabuni Feleshi na wa Biashara Henry Ngondo, walitembelea Kata ya Bwilingu kwenye Vitongoji vya Msolwa na Bwilingu, na kuwahamasisha walengwa hao umuhimu wa kununua vitambulisho hivyo ambapo kwa mwaka ni shilingi 20,000 tu.
Wakiwa na mwenyeji wao Hassani Mtamani zna wataalamu wake ngazi ya Kata, Makwinya aliwaambia umhimu wa vitambulisho hivyo kwa walengwa hao, ambapo mtu anayekuwanacho anafanya biashara yake kwa uhuru mkubwa pasipokubuguziwa.
"Faida nyingine ya kitambulisbo hiki ni kwamba unaweza kukitumia kukopa katika taasisi za kifedha, kwani ni moja ya uthibitisho wa mlengwa kwenye taaisi husika, niwaombe tuimie fursa hii tuliyopatiwa na Rais wetu mpendwa John Magufuli," alisema Makwinya.
Wakiongozwa na mwenyeji wao ofisa Mtendaji Kata Hassani Mtamani na maofisa wenzake ngazi hiyo, Makwinya aliongeza kuwa Serikali inapoandaa zoezi lolote linakuwa na maslahi kwa wananchi wake, na kwamba ni vema wakatumia fursa hiyo kwani hawajuu siku za usoni kitu gani kitatokea.
Wajasiriamali Kitongoji cha Msolwa Salumu Kakombe na Imani Masenga walisema kuwa wamepatiwa elimu juu ya zoezi hilo na umuhimu wake, lakini changamoto waliyonayo kipindi kilichopita cha ugonjwa wa Corona walikabiliwa na ugumu wa biashara.
Mwenyekiti wa Kitongoji hicho Peter Dimiango alimweleza Makwinya kwamba atakutana na wajasiriamali wote kitongojini hapo, ili kuwapatia elimu ya umuhimu na faida ya vitambulisho hivyo vilivyotolewa na Rais Dkt. John Magufuli.
Wakiwa Bwilingu, Feleshi na Ngondo waliwataka wajasiriamali kutambua juhudi zao za kuacha ofisi kuwafuata, lengo kuwaondolea usumbufu wa kwenda kwa Mtenda, benki au kwa Mawakala kulipia, badala yake wanahudumiwa walipo, ikiwemo elimu ya kulipia kwa njia ya simu zao za mkononi.
Mtamani alisema kuwa wanaendelea kutoa elimu lakini wanakabiliwa na changamoto ya mtandao katika kulipia, kwani kuna wakati mitandao ya simu inagoma hivyo kuaababisha malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara hao, na kwamba watalifanikisha kwa asilimia 100 kabla ya muda wa mwisho.
0 Comments