Na Amiri kilagalila,Njombe
Kijana aliyejulikana kwa jina la Patrick Ngailo
mkazi wa Mlangali wilayani Ludewa mkoani Njombe,anashikiliwa na jeshi la Polisi
kwa tuhuma za mauaji ya wakwe zake (mme na mke) akiwatuhumu ni washirikina
wanaomsababishia maradhi ya mara kwa mara.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema
kijana huyo alitenda kosa hilo katika kijijji hicho June 8,2020 majira ya saa
moja jioni lakini wananchi kwa kushirikiana na jeshi la polisi wamemkamata kijana
huyo.
“Baaa ya kufanya maauaji haya huyu mtu alikimbia
lakini wananchi walishilikiana na jeshi la polisi alikamtwa na sheria inafuata
mkono wake”
Awali kamanda Issa alisema jeshi hilo limefanya
uchunguzi na kubaini kuwa Ngailo alioa mtoto wa wazee hao lakini akapatwa na
maradhi ya mara kwa mara na kuchukuwa uamuzi wa kwenda mkwa mganga alikoelezwa
kuwa anapata maradhi kutokana na mke wake.
“Awali alioa mtoto wao baada ya kuoa mtoto huyo alienda
kwa mganga kutokana na kumwa umwa na akajulishwa yeye anaumwa kwasbabu ya huyo
mwanamke aliyemuoa akaamua kumuacha yule mwanamke,lakini cha ajabu kilichotokea
alikuwa anaendelea kuumwa na alichokifanya aliamua kwenda kufanya mauaji ya mke
na mume”alisema kamanda Issa
Aidha katika tukio jingine kamanda Hamis amesema lipo
tukio jingine lililotokea hivi karibuni mkoani Njombe la kuuawa kwa mwanaume
mmoja kutokana na kushambuliwa na vitu vyenye ncha kali akiwa amelala hali iliyofanya
jeshi hilo kuwashikilia mama na watoto wa familia hiyo.
“Kuna tukio jingine la mauaji yenye utata ambalo
baba na mama walilala katika nyumba moja lakini vyumba tofauti na asubuhi
walipoamka baba alikuwa amefariki na kufariki kwenyewe kumetokana na
kushambuliwa na vitu vyenye ncha kali,na hivi tunavyoonge mama na watoto
wameshikiliwa kwa kuwa mauaji hayo yanaonekana yamefanywa na wanafamilia,jeshi
la polisi linaenelea na uchunguzi na ukikamilika wahusika tutawafikisha kwenye
vyombo vya sheria”alisema kamanda
Vile vile kamanda wa Polisi amesema jeshi hilo
linawashikilia vijana wa mashambani waliomsababishia kifo kiongozi wao kutokana
na kununua Sola huku vijana wake wakishindwa kuridhika.
“Huko maeneo ya mashambani kuna kiongozi wa Vibarua
wa mashambani ambaye huwagawia mshahara wenzake lakini alinunua Sola ya
kumulika mashambani bila wafanyakazi wenzake kuridhika,ukatokea ugomvi
ukapeleka huyu kiongozi akafariki”alisema Issa
Kamanda wa polisi Hamisi Issa ametoa wito kwa
wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi.
0 Comments