Na Amiri kilagalila,Njombe
Wakazi wa mitaa ya Sido na Buguruni halmashauri ya mji wa Njombe wameshindwa kuzuia hisia zao baada ya kukamilika ujenzi na kuzinduliwa kwa zahanati ya mitaa hiyo ambayo ujenzi ujenzi wake umesuasua kwa zaidi ya miaka 9.
Ujenzi huo ulioghalimu zaidi ya Mil 110 umechukua muda mrefu kukamilika kutokana na sababu mbalimbali matumizi mabaya ya fedha za ujenzi huku pia tofauti za kiitikadi zikitajwa kuwa kikwazo kikubwa katika eneo hilo.
Baadhi ya akina mama walioshiriki uzinduzi wa zahanati hiyo akiwemo Riziki Chapile na Lustika Mtundu wanasema licha ya kuwa ndani ya halmashauri ya mji lakini wamekuwa wakipata shida kufuata huduma za matibabu nje ya mitaa yao katika kituo cha afya cha Njombe Mjini na hospitali ya wilaya Kibena hali ambayo imekuwa ikihatarisha maisha ya wajawazito nyakati za usiku.
Afisa mtendaji wa mtaa wa Sido Clara Mpete
katika taarifa ya ujenzi wa zahanati hiyo amesema imejengwa kwa michango mbali
mbali ikiwemo ya wananchi kwa zaidi ya shilingi milioni 50,mchango wa
Mbunge,Madiwani na Serikali hadi kukamilika kwake imetumia zaidi ya Shilingi milioni 100
“Jengo hili limeghalimu jumla ya shilingi milioni mia moja na kumi na saba elfu na mia tatu,lakini kwa sasa shughuli zilizobakia ni pamoja na ujenzi wa uzio katika shimo la taka ngumu”alisema Clara

Katibu wa Afya mkoa wa Njombe Frank Mhilu
anasema kuwa kukamilika kwa zahanati hiyo kunafanya mkoa kufikisha zahanati
zaidi ya 240 ambazo zinakwenda kupunguza changamoto ya upatikanaji wa huduma za
afya kwa kiasi kikubwa.
“Serikali haijaishia hapo kuwasaidia
wananchi,imetoa shilingi zaidi ya bioni saba kwa ajili ya ujenzi wa hospitali
ya Rufaa ya mkoa ipo kule Mgodechi,na jumla ya zahanati 243 lakini leo baada ya
uzinduzi wa zahanari hii tumeingiza zahanati ya 244”alisema Frank Mhilu
Dokta Isaya Mwasubila ni mganga mkuu wa
halmashauri ya mji wa Njombe anasema zahanati hiyo imeanza kutoa huduma zote za
msingi katika ngazi ya zahanati huku zoezi la ukamilisha kwa hatua
nyingine likiendelea.
nyingine likiendelea.
“Hapa pia tutazalisha akina mama,huduma
ya maabara ipo,ya chanjo ipo,huduma za virusi vya ukimwai pia iko hapa”alisema
Mwasubila
Akizindua zahanati hiyo Mbunge wa jimbo
la Njombe mjini Edward Frans Mwalongo anasema kuwa katika sekta ya afya jimbo
lake limekosekana zahanati katika vijiji takribani vitatu pekee kati ya vijiji
44.
“Tutafika mahala halmashauri ya mji wa Njombe tutakuwa na zahanati kila kijiji kwasababu sasa hivi tumebakiza karibu na vijiji vitatu na vyote vipo kwenye hatua mbali mbali,lakini zahanati hii imechelewa kukamilika ila kwa maana ya huduma ni daraja la kwanza”alisema Mwalongo

0 Comments