Walimu nchini wamehimizwa kuendelea kuchukua tahadhari katika kipindi hiki cha ugonjwa wa corona ili kuhakikisha masomo yatakaporejea wanakuwa salama kwa ajili ya kufundisha wanafunzi.
Katibu Mkuu wa chama cha walimu Tanzania CWT Deus Self amesema kuwa katika kipindi hiki walimu wanatakiwa kuchukua tahadahari ya kujikinga na ugonjwa wa homa ya mapafu nchini pamoja na kuendelea kutoa elimu kwa jamii inayowazunguka.
Ameongeza kuwa wanafunzi wanahitaji maarifa kutoka kwa walimu hivyo ni wajibu wao kuhakikisha shule zitakapofunguliwa wanakuwa salama.
Katika hatua nyingine amezungumzia elimu ya Mtandao ambapo wamesema itawasaidia wanafunzi kupata maarifa hususani kwa madarasa yenye Mitihani wakiwa nyumbani katika kipindi hiki cha kupambana na ugonjwa wa COVID- 19.
Hivi Karibuni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amelitaka Baraza la Mitihani Tanzania(NECTA) na Taasisi ya Elimu Tanzania kuhakikisha utaratibu wa kufanya marejeo ya mitihani ulioanza kwa kidato cha sita uhusishe madarasa yote yanayotarajia kufanya mitihani ya Taifa na kuwataka wanafunzi kuzingatia ratiba ya masomo inayotolewa ili wasikose vipindi vinavyorushwa kwenye redio,runinga na mitandao ya kijamii.
0 Comments