Wafanyabiashara wa Halmashauri ya jiji la Dodoma wameshauriwa kuendelea kufanya biashara zao kwa njia ya haki na uadilifu na sio kujipatia faida kwa njia ya udanganyifu.
Wito huo umetolewa na AFisa Masoko wa Halmashauri ya jiji la Dodoma Bwana James Yuna wakati akizungumza na kituo hiki kwa njia ya simu.
Wakati huo huo, amewataka wafanyabiashara hao kutopandisha bei ya bidhaa za vyakula katika kipindi hiki cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani na atakaye bainika amepandisha bei hatua za kisheria zitachukuliwa.
Amesema kuwa ikiwa wameweka utaratibu huo katika masoko juu ya kutopandisha bei ya bidhaa, si jambo jema kwa wafanyabisha kupandisha bei katika kipindi hiki huku akiendelea kufafanua kuwa tayari wamekwisha walekeza wafabiashara.
Pia, Bwana yuna ameendelea kusisitiza kuwa zipo sheria za kawaida ambazo mfanyabiashara azijue kwani katika masoko mengi biashara huwa zina bei elekezi hivyo atakeya pandisha ni lazima atawajibika kwa sheria za nchi zilizopo.
Hatahivyo, katika kipindi hiki ambacho Tanzania imekumbwa na ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (COVID-19) amewashauri wafanyabisha kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo kwa kufuata maelekezo yote ambayo yametolewa na wizara ya Afya.
0 Comments