Na Jackline Kuwanda, DODOMA.
Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya wakunga ambayo huadhimishwa kila Mei 5,Muuguzi na Mkunga wa hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo jijini Dodoma kwa upande wa mama na mtoto Angela Peter Aweda amesema kuwa wameendelea kuchua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (COVID-19) pindi wanapo wahudumia wagonjwa wao.
Aweda amesema kuwa watoa huduma wamekuwa wakijikinga kwa tahadhari kubwa wakati wa utoaji wa huduma pamoja na wagonjwa ambao wanawahudumia wahudumia
Wakati huo amewashauri wakina mama wanaonyoshesha kuendelea kuchukua tahadhari kwa kufuata maelekezo yanayotakiwa lengo likiwa ni kumlinda mtoto asikumbwe na maradhi hayo wakati kunyonya huku akisema kuwa wamepunguza idadi ya ndugu wanao kwenda kusalimia wagonjwa lengo likwa ni kuepusha misongamano isiyo ya lazima ambayo inaweza kusababisha kuongezeka kwa mambukizi.
Aweda ameendelea kuwasisitiza wakina mama ambao wamekwisha kujifungua na wako majumbani kupunguza idadi ya watu waokwenda kuwatembelea kwani hiyo itasaidia kumuepusha mama pamoja na mtoto kumkinga kupata ugonjwa wa corona.
Pia, amesema watoto wadogo wako hatarini kupata uonjwa huo kutokana na kinga zao kuwa chini amesema.
Hatahivyo, Aweda amesema katika siku hii ya mkunga kimataifa wanachojivunia kuzuia vifo vya mama na mtoto huku wakiendelea kutoa huduma kwa kufuata miongozo ya wizara ya Afya .
Kauli mbiu ya mwaka huu ya Siku ya Kimataifa ya Wakunga ni, "Wakunga, mama na familia washirika wa maisha."
0 Comments