TANGAZA NASI

header ads

Viongozi wa dini waendelea kusisitiza jamii kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Corona

 

Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.

Viongozi wa dini wameendelea kuwasisitiza waumini na jamii kuendelea kuchukua tahadari zote zinazoshauriwa na wataalamu wa afya katika kujikinga na virus vya corona licha ya takwimu kuonesha kuwa maambukizi yameshuka kwa kiasi kikubwa hapa nchini ili maabukizi hayo yaweze kupotea kabisa ndani ya aridhi ya Tanzania.

akizungumza wakati wa ibada ya jumapili na ikiwa ni siku ya mwisho ya maombi ya shukrani kwa Mungu yaliyotangazwa na Rais Dkt John Mgufuli askofu wa kanisa la Mlima wa Moto jimbo la Kati na Nyanda za juu kunisi Slivanus Komba amesema ni lazima wananchi waendelee kuchukua tahadhari licha ya kugonjwa kupungua.

“Nipende kuitumia madhabau hiikumpongeza Rais Jonh Magufuli kwa kuwa na ufahamu mkubwa juu ya kupambana na Ugonjwa wa Corona kwa kutambua kuwa silaha kubwa na ya pekee ya kutokomeza ugonjwa huo ni kufanya maombi.

“Unaweza kujiuliza kama ugonjwa hauna tiba nini kingesababisha ugonjwa kupungua na njia pekee iliyosababisha ugonjwa kupungua ni maombi ya watakatifu kufanya maombi watakatifuu na wenye hofu ya Mungu” amesema askofu Komba.

Mbali na kuwataka kuendeleza maombi pia askofu huyo amesema ugonjwa wa Corona hauwezi kuzuiliwa kwa risasi wala askari wa uhamiaji badala yake kinachotakiwa ni kuendeleza maombi na kufuata taratibu zote zinazotolewa na wataalamu wa afya.

Katika ibada hiyo amesema kuwa jambo pekee ambalo limefanywa na rais wa Tanzania juu ya kutokufunga makanisa na misikiti ndiyo sababu kubwa ambayo imepelekea kupungua kwa wagonjwa wa Corona nchini.

Amesema Rais Dkt Magufuli ni jasili na  Rais wa mfano na mcha Mungu kwa kuwa na uwezo kuzuia mikusanyiko yote lakini kutokufunga nyumba za ibada ni ujasili mkubwa na wakuigwa na mataifa mengine.

Amesema licha ya kelele nyingi lakini hakubadali msimamo wake na hatimae kumaliza salama bila madhara ambayo yalitegemewa au yaliyotabiliwa na baadhi ya watu wa mataifa ya nje ya Afrika ambao walitabili kuwa Afrika ingekuwa na wagonjwa wengi.

''Watu walipiga kelele sana kuhusu msimamo wa Rais wetu lakini hakuyumbishwa na kelele hizo, na  kuna watu walitabili kuwa Afrika maiti za watu zingeokotwa nyingi lakini sivyo ilivyotokea, bado baada ya kutangaza maombi na Mungu amejibu akatangaza siku tatu za shukrani, kweli huyu mtu mcha Mungu'' amesema.

Post a Comment

0 Comments