Na Jackline kuwanda, DODOMA
Ajali za Barabarani zimetajwa kuwa kama sababu namba moja ya
vifo kwa watoto wa umri kati ya miaka 5 hadi 14 pamoja na vijana wa umri kati
miaka 15 hadi 29 ambao ndio nguvu kazi ya Taifa.
Takwimu zinaonesha kuwa bado idadi ya vifo na majeruhi ni
kubwa licha ya juhudi zinazofanyika kwani ajali hizo zimekuwa zikiigharimu
serikali kurekebisha miundombinu,kufanya maokozi,kupoteza nguvu kazi ya Taifa
na vifaa tiba Hospitalini.
Akifungua kongamano la Usalama wa Barabarani jijini Dodoma
ikiwa ni Muungano wa Asasi za Kiraia zinazo shawishi Maboresho ya sheria ya
usalama Barabarani,Waziri wa mambo ya ndani ya Nchi Mh George Simbachawene
amesema kuwa wanachi wengi wamekuwa wakipoteza wapendwa wao katika ajali na
baadhi kusababishiwa ulemavu na majereha ya kudumu hivyo kupitia wizara yake
amesema ipo katika mchakato wa kurekebisha sheria ya usalama barabarani 1973
ili iweze kuendana na mahitaji ya sasa.
Amesema kama serikali wanayo nia ya dhabiti ya kuhakikisha
kwamba ajali zinapungua kwa asilimia 50% ifikapo 2030 kama ambavyo wameahidi
katika mikataba ya kimataifa na kama matakwa ya sheria za kimataifa zinavyosema
huku akitoa wito kwa madereva wanao endesha magari kuzingatia sheria za
barabarani kwani wako madereva wanao endesha kwa mwendokasi ,wakiwa wamelewa na
ameliagiza jeshi la usalama barabarani kuchukua hatua kali dhidi ya wale wote
wanaokiuka sheria za usalama Barabarani.
Akizungumzia masuala ambayo mtandao unafanyia uchechemuzi
Rose Reuben ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA amesema kuwa
mtandao unafanya uchechemuzi juu ya mfumo bora wa kisheria juu usalama wa
barabarani ili kuhakikisha kuwa ajali za Barabarani zinapungua ikiwa ni pamoja
na majeraha yatokanayo na ajali barabarani pamoja na vifo.
Amesema mtandao ulianzishwa kwa malengo kadhaa ikiwa ni
pamoja na kuwa na sauti ya pamoja katika kuendesha kampeni ya kushawishi
maboresho ya sheria ya usalama barabarani .
Hatahivyo, Takwimu za Shirika la Afya ulimwenguni zinaonesha
kuwa zaidi watu 1,350,000 hufariki kwa ajali za barabarani duniani kote.
0 Comments