TANGAZA NASI

header ads

Chalinze wafikilia kununua Greda



Na Omary Mngindo, Lugoba

HALMASHAURI ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, imeanza kufikilia hatua ya kununua greda watalotumima kuchonga barabara zilizomo ndani ya Halmashauri yao.

Hatua hiyo inalenga kusaidia juhudi za serikali kuu, kupitia wakala wa ujenzi wa Barabara za mijini na vijijini (TARURA) chombo kilichoundwa kisheria kusimamia kazi za uchongaji wa barabara zilizomo ndani ya Halmashauri hiyo.

Mpwimbwi alitoa kauli hiyo katika Baraza la Madiwani la kawaida, likihudhuliwa na mbunge wa Jimbo Ridhiwani Kikwete, wa Viti Maalumu Subira Mgalu (Naibu Waziri wa Nishati) na wataalamu mbalimbali, ambapo alisema lengo ni kukabiliana na changamoto za miundombinu.

Kauli ya Mpwimbwi imefuatiwa na taarifa ya Meneja wa TARURA Henrico Shauri, iliyoelezea changamoto ya fedha inayoikabili ofisi yake, ambapo alisema fedha wanazopatiwa hazikidhi kutengeneza barabara zilizopo, huku akisema ameshaomba fedha halmashauri kupitia ofisi ya Mkurugenzi lakini hajapatiwa majibu.

"Ndani ya Halmashauri kuna barabara nyingi hazipitiki, isitoshe tumesikia taarifa ya Meneja wa TARURA ikisema kuwa inapata fedha kidogo, ambazo hazikidhi mahitaji, naona kama ikiwezekana kuna haja ya kununua greda letu litalosaidia zoezi hilo," alisema Mpwimbwi.

Kwa upande wake Ridhiwani amemtaka Meneja wa TARURA kuacha kujifungia ifisini wanapopata fedha japo kidogo, badala yake wawashirikishe Madiwani ili wawasaidie ushauri wa maeneo gani waelekeze katika kuchonga au kujenga barabara husika.

"Nikuombe Meneja Shauri, mnapopatia fedha jaribuni kushirikisha Madiwani, hatua hii itaisaidia ofisi yako kuondokana na malalamiko yanayoelekezwa kwenu, leo umeelezea miradi iliyotengewa fedha, lakini barabara za Talawanda zimepewa kipaumbele kikubwa," alisema Ridhiwani.

Nae Mgalu alichangia mada alipongeza Seeikali kwa kuunda chombo hicho, na kwamba wakiwa Talawanda alishawahi kugusia jambo hilo huku akitolea mfano wa kazi nzuri zinazofanyika chini ya REA na RUWASA vyombo vinavyofanya kazi nzuri.

Kaimu Mkurugenzi Zaynabu Makwinya aliliambia Baraza hilo kwamba wamepokea maoni na ushauri mbalimbali uluitolewa na wajumbe, na kwamba wamezipokea na kuahisi watakwenda kuzifanyiakazi.

Post a Comment

0 Comments