TANGAZA NASI

header ads

Ndugu wapata hasira,wafyeka Shamba la Ndizi za Mjane kwa kushindwa kesi Mahakamani






Shamba la mama Mjane anayejulikana kwa jina la Angelina Mwita mkazi wa kijiji cha Ntagacha kata ya Ganyange wilayani Tarime limefyekwa na watu wanaodaiwa kuwa ndugu wa Mmewe ambaye kwa Sasa ni Marehemu baada ya kushindwa kesi katika Mahakama tofauti

"Mme wangu tangu amefariki nimeanza kufukuzwa na ndugu zake kwa kutaka kuninyanganya hilo shamba lakini tumeanzia Baraza la kata nikashinda kesi wakakata rufaa Mahakama ya wilaya nikashinda lakini nikija kulima nafukuzwa kwa  Mapanga pia walishanishambulia na watoto wangu kuhumizwa Sana" alisema Angelina Mwita

Aidha ameiomba Serikali ichukue eneo hilo na kuliuza ili aweze kununuliwa sehemu nyingine ambayo ataishi kwa amani na watoto wake, anao wasomesha kupitia shamba hilo la Migomba.

Amesema mtoto wake mmoja yuko kidato cha tatu na mwingine amefaulu kwenda kidato cha tano hivyo atashindwa kuwasomesha kwakuwa hana fedha wala mtu wa kumsaidia kwa kuwa ndugu wa mme wake wanamfukuza.

Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Tarime Mhandisi Mtemi Msafiri ametembelea eneo hilo na kulaani vikali unyama huo na kuahaidi kuwasaka  wote waliohusika na tukio hilo ili kuwachukulia hatua.

Post a Comment

0 Comments