Na Gabriel Kilamlya,Njombe
Wananchi mkoani Njombe wamelalamikia kuchelewa
kusikilizwa kwa Mashauri ya migogoro ya ardhi na kupelekea kuwaathiri kiuchumi
wakati wakiendelea kufuatilia mashauri yanayosikilizwa na baraza ya ardhi.
Hayo yamebainishwa na baadhi ya wananchi wanaofika
katika mabaraza ya ardhi yanayosuluhisha migogoro ya ardhi mkoani Njombe ambapo
miongoni mwao akiwemo Remigius Ilomo na Geofrey Msambwa wamezungumzia kero
wanayoipata na Kwamba Kumekuwa Kukiwaongezea Gharama kubwa pindi wanapofuatilia
mashauri yao kutokana na kesi kuahirishwa mara kwa mara.
“Kesi moja inaweza ikachukua miezi sita mpaka saba
kiasi kwamba uchumi unashuka kwasababu shughuli kwenye maeneo yenye kesi
zinasimama,halafu inaongeza vita mbali mbali kwasbabu watu tunabaki na chuki na
hatuwezi tukagombana na wahuduma”alisema Geofrey Msambwa
Ruth Mdugo ni mkazi wa kijiji cha Imalinyi wilayani Wanging'ombe
mkoani Njombe ambaye anasema kilio chake kikubwa ni kesi yake kuahirishwa mara
kwa mara hatua ambayo inampa wakati mgumu kwa kuwa imekuwa ikimpa changamoto
kubwa katika suala la kiuchumi.
“Kinachonisumbua ni kwasababu pesa hamna na kipindi
hiki imetoka kunyesha mvua,umri huu hata pesa sina natembea kwa kuhangaika kama
hivi juzi nimeondaoka nyumbani kwa mguu nimelala njiani jana,ndio nimefika
jioni hapa kiuchumi kwa kweli naathirika naomba mnisaidie”alisema Ruth Mdugo
Kwa kuona matatizo kama hayo serikali kupitia wizara
ya Ardhi Nyumba na maendeleo ya makazi imelazimika kufungua ofisi za ardhi kila
mkoa kwa Tanzania Bara ambapo shughuli
zote za Ardhi zitakuwa zikipatikana mkoa husika.
Kamishina msaidizi wa Ardhi mkoa wa Njombe,
Christopher Mwamasage anasema kufunguliwa kwa ofisi hizo itakuwa mwarobaini
katika utatuzi wa migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ikilalamikiwa na watu wengi
kila pahala hapa nchini.
“Migogoro ya ardhi mingi ni uelea tu wa sheria
utakuta mtu anauza ardhi ambayo siyo ya kwakwe,na nimeorodhesha migogoro yote
mkoa wa Njombe ninaielewa ilivyo najua nitapambana nayo vipi na sio kuwa
migogoro ilikuwa haishughulikiwa ilikuwa inashughulikiwa”alisema Christopher Mwamasage
Kuhusu huduma zitakazotolewa na ofisi ya Ardhi mkoa
wa Njombe bwana Mwamasage amesema ni pamoja na upatikanaji wa hati za Ardhi.
“Kwa hiyo kila kitu kitaishia hapa hapa Njombe
hakuna sijui utaenda Dar es Salaam,Mbeya mambo yote yataisha hapa kwa hiyo
ufanisi utakuwa mkubwa na wananchi watanufaika sana”Aliongeza Christopher Mwamasage
Katika vikao vya bunge la bajeti vinavyoendelea
Bungeni Dodoma Waziri wa Ardhi Ameeleza Lengo la kufungua Ofisi hizo kila mkoa
ikiwa ni Hatua Mojawapo ya kupunguza migogoro ya Ardhi Hapa Nchini.
0 Comments