TANGAZA NASI

header ads

Corona yapindua soko la Nyanya Makambako



 

Na Clief Mlelwa,Makambako

Wafanyabiashara wa soko la Nyanya mjini Makambako mkoani Njombe wamesema kuwa wameathirika kwa kiasi kikubwa kiuchumi kutokana na janga la corona ambalo limesababisha wanunuzi wengi kutoka mikoa mbalimbali nchini kusitisha safari zao za kufika na  kununua zao hilo.

Wafanyabiashara wa soko hilo wamesema kwa sasa box moja la nyanya wanauza shilingi elfu tano,hadi elfu nane wakati walitakiwa waunze elfu ishirini hadi thelethini.

Aidha baadhi ya wakulima wa zao hilo la Nyanya wamesema kuwa kutokana na bei la zao hilo kushuka imesababisha washindwe kumudu ghalama za pembejeo za kilimo.

Naye mwenyekiti wa soko la Nyanya mjini Makambako Boscor Kitte amesema kuwa bei la zao hilo limeshuka kutokana na wafanyabiashara wengi kusitiza zoezi la kusafirisha zao hilo kwenda mikoa mingine.

Hata hivyo mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Makambako Hanana Mfikwa amewataka wafanyabiashara hao kuendelea kuchukua tahadhali na kueleza kuwa suala la kushuka kwa uchumi kwa sasa ni la taifa kwa ujumla.


Post a Comment

0 Comments