TANGAZA NASI

header ads

Hispania:Yaruhusu Watu kutembea nje kwa mara ya kwanza

 

Wakati huo huo baadhi ya  mataifa ya Ulaya  kwa tahadhari yalilegeza vizuwizi vya kutoka nje, wakati Urusi na Ujerumani zimeripoti ongezeko la maambukizi.

Wakati serikali zikitafakari kuondoa vizuwizi vya  kuwataka  wananchi  kubakia  majumbani ili kuanzisha tena  uchumi wao, maafisa nchini Marekani  wameleta  matumaini kiasi  kwa  kuidhinisha  dawa ya  majaribio  ili  itumike  kwa wagonjwa  wa ugonjwa wa  COVID-19

Uamuzi  huo  ulikuwa  wa  hivi  karibuni  kabisa   katika  hatua  za dunia  kutafuta  dawa  na  chanjo  kwa ajili  ya  virusi  vya  corona, ambavyo  vimesababisha  nusu  ya  binadamu  dunia kuwamo  katika  vizuwizi vya  kutoka  nje na  kuuweka  uchumi  wa  dunia  kuelekea katika  mporomoka  mbaya  kabisa  tangu mdororo  mkuu  katika miaka  ya  1930.

Virusi  sasa  vimewauwa  zaidi  ya  watu 242,000 duniani  kote, kwa  mujibu wa  idadi  iliyowekwa  pamoja  na  shirika la  habari  la  AFP, na  walioambukizwa  wanafikia  milioni 3.4  tangu kuzuka  mara  ya  kwanza  virusi hivyo nchini  China mwishoni  mwa  mwaka jana.

Kukiwa na  ishara  kwamba  janga  hili  linapungua  kasi  katika mataifa  yale yaliyoathirika zaidi , mataifa  ya  Ulaya  pamoja  na baadhi  ya  sehemu  za  Marekani  yameanza  kuondoa  vizuwizi kujaribu kurejesha  hali  ya  maisha  kuwa  ya  kawaida  katika uchumi  ambao ulioathirika  kutokana  na  wiki  kadhaa  za kufungwa.
 (Muungwana blog)

Post a Comment

0 Comments