Mdhibiti
na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali nchini Bw,Charles E Kichere akizungumza
na baadhi ya watumishi wa ofisi ya mkaguzi mkoa wa Njombe nje ya jingo jipya la
ofisi ya mkaguzi linalojengwa Lunyanywi mjini Njombe.
Mdhibiti
na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali nchini Bw,Charles E Kichere akikagua moja
ya chemba ya ofisi mpya za ukaguzi mkoa wa Njombe.
Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali nchini Bw,Charles E Kichere akikagua ubora na kuta za jengo la ofisi mpya za ukaguzi mkoa wa Njombe.
Mdhibiti
na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali nchini Bw,Charles E Kichere,Akipata
maelezo mafupi na mmpja wa ofisa ukaguzi mkoa wa Njombe juu ujenzi wa jengo
hilo jipya la ofisi za ukaguzi.
Muonekano
wa nje sehemu ya jengo la ofisi mpya za ukaguzi mkoa wa Njombe zinazojengwa
Lunyanywi mkoani Njombe.
Mdhibiti
na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali nchini Bw,Charles E Kichere,Akizungumza
na waandishi wa habari mara baada ya ukaguzi wa jengo la ofisi za ukaguzi
Njombe.
Na
Amiri kilagalila,Njombe
Mdhibiti
na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali nchini Bw,Charles E Kichere,amesema
ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa ofisi ya Taifa ya ukaguzi mkoa wa Njombe
inayoendelea kujengwa mkoani humo,huku akiagiza kukamilishwa kwa ofisi hizo
kabla ya mwezi wa sita ili ziweze kutumika.
Akiwa
katika eneo la jengo za ofisi hizo lililopo Lunyanywi halmashauri ya mji wa
Njombe,Kichere amesema anahitaji majengo hayo kukamilika kabla ya mwezi wa sita
ili watumishi wapate mazingira mazuri ya kufanya kazi.
“Majengo
haya ni mazuri na yanaendelea vizuri nadhani itabidi mwaka huu kabla ya mwezi
wa sita wamalizie kazi ndogo ndogo ambazo zimebaki ili tuingie kabla ya mwezi
wa sita”alisema Kichere
Vile
vile Kichere amesema ujenzi huo unaendelea katika mikoa mingine minne katika utekelezaji
wa matakwa ya kuwa na ofisi binafsi mikoa yote ya Tanzania.
“Kwa
hiyo tumekubalina na Serikali kwamba tuwe tunajenga ofisi kwa ajili ya sisi
kuwa na ofisi zetu,sasa hivi tunaendelea kujenga ofisi mkoa wa
Mara,Simiyu,Geita na hapa Njombe na ofisi zipo katika hatua mbali mbali za
kuhamia”alisema Kichere
Katika
hatua nyingine amesema ofisi ya Mkaguzi mkuu inategemea mwaka wa fedha
2020/2021 kuanza ujenzi wa ofisi katika mikoa mingine minne mara baada ya
kukamilisha katika mikoa ambayo tayari ujenzi unaendelea.
“Lakini
pia niishukuru Serikali tunapanga mwaka kesho kama mambo yatakuwa sawa tutaanza
kujenga ofisi zetu katika mkoa wa Mwanza ambako tumepanga,mkoa wa Tanga,Katavi
na mkoa wa Songwe ili kila mkoa tuwe na ofisi”aliongeza Kichere
Aidha
Bw,Kichere amesema ujenzi wa ofisi za ukaguzi kila mkoa ni kutimiza matakwa ya
viwango vya ukaguzi wa Kimataifa.
“Kwa
sasa hivi tuna miradi ya kujenga ofisi za ukaguzi katika mikoa yetu yote ya
Tanzania,ili kutimiza matakwa ya viwango vya ukaguzi wa kimataifa ambavyo
vinataka sisi tuwe na ofisi ya kwetu badala ya kuwa tunakaribishwa tunakaa kwa
wakaguliwa.Mfano ukienda Mara utakuta ofisi ya Mkaguzi iko ndani ya ofisi ya
mkuu wa mkoa ambaye ni mkaguliwa wetu”alisema tena Kichere
0 Comments