Na Jackline Kuwanda,DODOMA
Waandishi
wa habari Jijini Dodoma wamekishukuru Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake
(TAMWA) kwa kuwapatia mafunzo ya usalama wa kimtandao (Cyber Security Training)
kwani imekuwa ni njia moja wapo ya wao kufahamu matumizi sahihi ya mtandao.
Wakizungumza
mara baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo waandishi hao akiwemo Veronika komba
pamoja na Ronald Sonyo wamesema kuwa kupitia mafunzo hayo wamejifunza mengi
kikubwa watazingatia yale yote waliyofundishwa na wao kwenda kuwafundisha wengine
kuhusiana na matumizi mazuri ya mtandao hasa wakiwa kama wanahabari.
Godwin
Assenga ambaye ni mratibu wa mradi wa usalama wa kimtandao (Cyber Security
Training )kutoka TAMWA ambaye ndiye alikuwa akitoa mafunzo kwa waandishi wa
habari amesema kuwa mradi huo wameundaa kwa wanahabari ambao wamekuwa wakifanya
nao kazi kwa ukaribu baada ya kuona kuna ulazima wa kuhakikisha usalama kwa
wanahabari katika mitandao huku akieleza lengo la mafunzo hayo.
Akifunga
Mafunzo hayo mkurugenzi mtendaji wa TAMWA Bi Rose Reuben amewataka wanahabari
ambao wamepata mafunzo hayo kwenda kuyafanyia kazi katika maeneo yao.
Hatahivyo,wanahabari wameendelea kusisitizwa kuzingatia matumizi sahihi ya mtandaoni ili
matatizo mengine yasiweze kujitokeza kwani watu wengi wamekuwa wakifuatilia
mitandao hivyo kama mwandishi ataenda kinyume na matumizi mazuri ya mtandao
basi anaweza kukumbana na matatizo.
0 Comments