Shirika la Raleigh Tanzania limeanza utekelezaji wa Kampeni ya kitaifa kuhusu Uwajibikaji wa Jamii Kupitia Vijana.
kampeni hiyo ni sehemu ya Mradi unaoendelea mikoa ya Dodoma, Morogoro na Iringa Kwa kushirikiana na Halmashauri za Wilaya na Mkoa.
Shirika hilo pia linatekeleza mradi wa uwajibikaji wa jamii kupitia vijana ambapo mradio huo unatumia mfumo wa kujenga jamii adilifu mfumo ambao unashirikisha wananchi wenyewe kutafuta sulihisho la changamoto zinazojitokeza kwenye miradi au huduma katika jamii.
Akizungumza kwa Njia ya simu kupitia kipindi cha Maisha Breakafast kinachorushwa na kituo cha Radio Maisha Mkoani hapa, Afisa Mradi kutoka shirika hilo ambaye ameutambilisha mradi wa kampeni hiyo Onesmo Joel Mwandemele amesema kuwa lengo la mradi ni kuwapa nguvu wanawake,vijana pamoja na makundi ya watu wenye ulemavu kushiriki katika miradi ya maendeleo ambayo ipo katika maeneo yao.
Wakati huo huo, Amesema kuwa mpaka sasa kwa Mkoa wa Dodoma wamekuwa wakifanya kazi kwenye mitaa na vijiji sabini na mbili katika wilaya zote za Dodoma .
Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwa njia ya simu vijana wanaojitolea katika kampeni ya uwajibikaji wa jamii kupitia vijana na wanufaika wa mradi huo akiwemo Happy Nyoni mkazi wa wilaya ya kongwa Dodoma ambaye ni mratibu wa kampeni katika shirika hilo ameelezea uhamasishaji unaoendelea kwenye wilaya,vijiji na muitikio wa wanawake,vijana na watu wanaoishi na ulemavu huku Peter Taty wa kijiji cha Mundemu Wilaya ya bahi amesema anajisikia vyema kwa kufanya shughuli inayo inufaisha jamii.
Wilson Dau Kihogo ni mtendaji wa kijiji cha Mudemu wilayani Bahi yeye ameelezea kikundi kazi kilicho undwa kwenye jamii yake na namna kinavyofanya na matokeo yake mpaka sasa huku Jane Pantaleo ambaye ni mratibu wa kampeni wilaya ya Dodoma mjini akizungumzia hali ilivyokuwa zamani kabla ya kuanza mradi huo na mwako wa makundi lengwa.
Kuanzia mwaka 2018 -2020 mradi huo umeweza kufikia vijiji/ mitaa 179 katika mikoa mitatu (Dodoma, Iringa na Morogoro).
0 Comments