Wazazi na walezi wilayani Njombe wametakiwa kuwahimiza watoto wao kujisomea wakiwa nyumbani katika kipindi hiki nchi ikiwa katika mapambano dhidi ya virusi vya corona.
Akizungumza na jana katika kikao wa wadau mbalimbali wanaotoa huduma za kijamii wakiwemo viongozi wa dini,mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri,alisema ingawa shule zimefungwa lakini wazazi na walezi kipindi hiki ambacho watoto wapo nyumbani wanawajibu wa kuwahimiza kujisomea.
"Kweli shule zimefungwa licha ya katazo niwaombe wazazi na walezi muwahimize watoto kujisomea wakati huu wakiwa nyumbani kwa sababu muda wowote ugonjwa huu ukiisha wanapaswa kurudi shuleni"alisema Ruth.
Naye mchungaji kiongozi wa kanisa la Efatha Boniface Mwakisalu alisema wachungaji wanapaswa kuondoa ibada zinazohusisha watoto na badala yake wabaki na wanaojitambua.
"Wachungaji wote wabadilike waondoe ibada kwa watoto ili waweze kuwa salama na karantini ya nyumbani ni lazima,watoto wadhibitiwe,wanafunzi watulie wasome wakichoka wapumzike wakiwa ndani naomba hili tuzingatie"alisema Mwakisalu.
Pia mchungaji Mwakisalu aliwaomba wachungaji wabadilishe aina ya kuombea waumini wao kwa kuweka mikono ili kujiepusha na maambukizi ya virusi vya corona.
Naye Dismas Manyika mtoa huduma ya vyakula mjini Njombe alisema bado kuna changamoto kwa wananchi kunawa mikono huku wengine wakiwa na lugha mbaya.
0 Comments