TANGAZA NASI

header ads

Ulega ataka miradi ikamilike



Na Omary Mngindo, Mkuranga

Mbunge wa jimbo la Mkuranga mkoa wa Pwani ambae ndio naibu wa waziri wa mifugo na uvuvi Abdallah Ulega, amefanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya idara ya afya. 

Ziara hiyo mbali ya kujionea maendeleo ya miradi, pia kujiridhisha matumizi ya oesa kutoka halmashauri pamoja na serikaali kuu namna zilivyotumika kwenye miradi husika, huku akitoa maagizo ya kukamilika mingine ambayo bado.

Akiwa kwenye ziara hiyo, amejionea maendeleo ya ujenzi katika maeneo matano, huku akitoa maagizo kwa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri mhandis Mshamu Munde na wataalamu wake, ukamilishwaji wa haraka wa miradi hiyo. 

Mradi iliyotembelewa ni ujenzi wa zahanati za kimanzichana magharibi na mwarusembe ambazo zipo hatua ya unaliziaji, ujenzi wa wodi ya wazazi hospitali ya wilaya ambayo ipo katika hatua ya kupauliwa.

Pia amekagua ujenzi wa kituo cha afya vikindu ambacho kinakaribia hatua hatua ya linta, sanjali na zahanati ya mwandege ambayo nayo ipo kwenye hatua ya kumalizia. 

"miradi hii ya idara ya afya ni miongoni mwa miradi 34 ya zahanati zilizoanzishwa kipindi cha miaka minne ya serikali ya awamu ya tano ambazo zipo katika hatua tofauti za ujenzi," alisema ulega.

Aidha naibu waziri huyo alitembelea zahanati tano zinazoendelea kujengwa, huku zingine tano zikiwa zimefunguliwa katika kipindi hiki, ambazo ni chamgoi, kisemvule, mkanoge, malela na mfulu mwambao.

"ujenzi wa wodi ya wazazi hospitali ya wilaya yenye uwezo wa kuhudumia wazazi 80 kwa pamoja, upatikani wa x-ray na utra sound ni miongoni mwa mafanikio kwenye idara ya Afya kwa kipindi hiki cha miaka minne ya serikali ya awamu ya tano," alisema ulega. 

Pia ulega alisema kuwa vituo viwili vya afya vimeboreshwa ambavyo ni cha mkamba na kisiju, huku kituo kipya cha vikindu kikiendelea na ujenzi wake, ambapo pia ametumia fursa hiyo kusisitiza taadhali ya ugonjwa wa corona.

Katika ziara hiyo aliongozana na mkurugenzi mtendaji mhandisi mshamu munde, katibu mwenezi wa ccm wilaya Beni Mkulya, mhandisi wa ujenzi wa halmashauri na mganga mkuu wa hospitali ya wilaya.

Post a Comment

0 Comments