TANGAZA NASI

header ads

Kongwa:Wananchi walalamikia uongozi kwa kutoshirikishwa kwenye maamuzi




Na Jackiline Kuwanda,Dodoma

Wananchi wa kijiji la Mbande kata ya sejeli wilayani Kongwa wamelalamikia uongozi kijiji hicho kutowashirikisha katika mambo ya maamuzi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa kituo cha afya na kituo cha polisi.

Pia wamemlalamikia  mwenyekiti wa kijiji cha Mbande kwa kutokusoma mapato na matumizi katika mikutano ya hadhara.

Baadhi ya wananchi akiwamo Abeid Idani Abeid wamesema kuwa mfumo wa uongozi katika kijiji hicho hauko sawa kwami uko kimaslahi zaidi kwa baadhi ya watu kwani mikutano yao ya kijiji haiitishwi kwa wakati na hata ikiitishwa mapato na matumizi ya kijiji chao huwa hayawekwi wazi.

Kutokana na malalamiko hayo kutoka kwa wananchi mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya kongwa Dkt,Omary Nkullo amesema kuhusiana na suala la mapato na matumizi  wamekwisha kutoa maelekezo kwa watendaji wote huku akiwaasa wananchi kuhudhuria mikutano ya vijiji inayoitishwa  hasa ya kusoma mapato na matumizi kwani taarifa mbalimbali za maendeleo hupatikana katika mikutano hiyo.  

Akizungmzia changamoto hiyo ambayo imetolewa  na wananchi wa kijiji hicho wilayani humo, mkuu wa wilaya hiyo Deogratius Ndejembi amesema kuwa malalamiko hayo ambayo yametolewa na wananchi hayajafika katika ofisi yake wala kwa mkurugenzi iwe kwa maandishi au kwa wao kufika kuyasema.

Post a Comment

0 Comments