TANGAZA NASI

header ads

Wafanyabiashara minadani waomba kufikishiwa Barakoa


OPERESHENI ONDOA MIFUGO KAGERA YASONGA MBELE SASA NG'OMBE WASAKWA ...
Handeni

Wafanyabiashara  wa mnada wa mifugo Ndelema wilayani Handeni mkoani Tanga,wamewashauri wadau wanaosambaza barakoa kuwafikishia wananchi kwenye maeneo ya minada iliyoko vijijini,kwani wapo ambao wanapenda kujikinga ila hawafahamu ni wapi watapa vifaa hivyo.

Wakizungumza mnadani hapo wakati wa kampeni ya kupewa elimu dhidi ugonjwa wa Corona iliyokuwa inafanywa na shiriki lisilo la serikali la Dorcas relief and development,wafanyabiashara hao walisema,wanapenda nao kujilinda na kuchukua tahadhari ila changamoto ni kukosekana barakoa hizo kwenye maeneo yao pamoja na bei kubwa hali ambayo inawafanya kuingia kwenye makundi bila kinga hizo.

Mwenyekiti wa wauza mifugo mnada wa Ndelema Abdi Mhandeni amesema kila mfanyabiashara anatakiwa kuhakikisha anajikinga na maambukizi dhidi ya virusi vya ugonjwa wa corona kwa kufuata maagizo ya serikali kupitia wizara ya afya kwa kunawa mikono na kuvaa barakoa ili kujikinga.

Afisa mradi wa shirika la dorcas relief and development orgenes kihampa,amesema wafanyabiashara hao wanatakiwa kuchukua tahadhari mapema,kwani ugonjwa ukifika maeneo hayo hata mnada unaweza kufungwa kwani  kuna wanunuzi na wauzaji kutoka maeneo kama zanzabar, mombasa, na mikoa mbalimbali ya tanzania, hivyo uvaaji wa barakoa na kunawa mikono ni jambo muhimu.

Shirika hilo limetoa elimu kwa wananchi katika kata zaidi ya nane dhidi ya ugonjwa wa corona,kujua dalili na jinsi ya kujikinga na covid-19.

Post a Comment

0 Comments