Na Ibrahim
Mlele,Njombe
Kutokana
na elimu ya namna ya kujikinga na ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayotokana na
virusi vya Corona (COVID-19) kutowafikia vyema wananchi waishio maeneo ya
vijijini wadau mbalimbali wa maendeleo mkoani Njombe wameanza zoezi la kwenda
kutoa elimu kwa wananchi juu ya kujikinga na ugonjwa huo.
Miongoni
mwa wadau hao ni Johson Mgimba na Lawi Mnyanga ambao wamefika katika kata ya Madilu wilayani Ludewa mkoani Njombe
na kutoa elimu kwa wananchi mbalimbali kupitia maeneo ya ibada ambapo
wamewataka wananchi kufuatilia vyombo mbalimbali ili kufuatilia taarifa za
wataalam wa afya ili kujikinga na virusi vya Corona.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa utume na uinjilisiti taifa kanisa la Anglican Tanzania,
Nicolaus Mgaya amewataka waumini wa kanisa hilo kufuata sheria za wataalam wa
afya ikiwemo kuvaa barakoa wawapo kwenye maeneo ya ibada pamoja na kukaa umbali
wa mita moja ili kukabiliana na ugonjwa huo.
Baadhi
ya wananchi waliofikiwa na elimu hiyo wamewashukuru wadau wa maendeleo wakiwemo
vijana kutoka kata ya Madilu huku wakiwa tayari kukabiliana na ugonjwa huo kwa kufuata
kanuni za afya.
0 Comments