TANGAZA NASI

header ads

Wanafunzi wawili wa familia moja wauawa kikatili mkoani Njombe




Na Amiri kilagalila,Njombe

Vijana wawili wa familia moja wameuawa kikatili kwa kupigwa na vitu vizito kichwani usiku wa kuamkia april 27 katika kijiji cha Kipengele kilichopo wilayani Wanging'ombe mkoani Njombe

Akizungumzia tukio hilo kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe Hamis Issah amesema vijana waliouwawa ni
Felis Frank Chaula(20) mwanafunzi wa chuo cha uhasibu Dar es salaam pamoja  na Fabio Frank Chaula mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari Mount Kipengele ambapo wote ni watoto wa mzee Frank Chaula ambaye ni kiongozi wa kijijini hapo.

Kamanda Issah amesema katika tukio hilo ambalo limetokea katika nyumba ya biashara ya familia hiyo , watu saba wamekamatwa ili kusaidia upelelezi wa tukio hilo huku pia kamati za ulinzi na usalama kutoka ngazi ya wilaya na mkoa zikilazimika kukutana kwa dharura kujadili namna ya shughulikia tukio hilo.

Mauaji ya kikatili yaliofanywa kwa vijana hao ambao ni wanafunzi unamfanya mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka kushindwa kujizuia na kuagiza kuchukuliwa kali hatua kali dhidi ya wahalifu watakapobainika.

Baadhi ya wakazi ambao wamefika katika eneo la tukio wanasema kumekuwa na matukio ya mauaji mabaya ya kufatana takribani 7 hivyo wanaiomba serikali kuchukua hatua madhubuti za kuwabaini wahusika .


Post a Comment

0 Comments