Serikali ya Uturuki imetuma msaada wa madawa na vifaa vya matibabu nchini Uingereza katika juhudi za kupambana na virusi vya corona nchini humo.

Wizara ya afya nchini Uturuki imesema vifaa  hivyo ni kwa ajili ya ushirikiano katika mapambano dhidi ya virusi vya corona.

Msaada huo ni pamoja na  barakoa  aina ya N95 na  vifaa vingine ambavyo hutumiwa katika  kuzuia maambukizi  ya Covid-19.

Mpaka sasa serikali ya Uturuki imetuma  misaada ya madawa na vifaa vya matibabu nchini Italia, Uhispania, Mekedonia Kaskazini, Montenegro, Serbia, Boznia na Kosovo pamoja na Uingereza.