Rais wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia amesema ligi kuu ya Vodacom haitaendelea baada ya siku 30 zilizotolewa awali,kuwa watasubiri maelekezo mengine kutoka kwa serikali

Siku 30 za kusitisha shughuli zote za michezo yenye mikusanyiko zilizotolewa na Waziri Mkuu Mh Kassim majaliwa, zitamalizika April 17 mwaka huu.

Karia amesema hakuna mchakato wowote kuhusu ligi hiyo ambao unaendelea mpaka pale Serikali itakapotoa maelekezo.

Kuna uwezekano mkubwa ligi haitarejea siku za karibuni kutokana na kuongezeka kwa kasi ya maambukizi ya virusi vya corona nchini.

Katika taarifa iliyotolewa na serikali imebainisha kuwa mpaka sasa wagonjwa wa corona nchini Tanzania wamefika 32,waliofariki ni watatu wakati wagonjwa waliopona ni watano,na wengine wakiendelea vizuri