Na
Amiri kilagalila,Njombe
Taasisi
ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU mkoa wa Njombe imefanikiwa kuokoa
Bilioni 1,769,161,693.31 kutokana na chunguzi zinazohusu AMCOS na SACCOS mkoani
humo.
Mkuu
wa TAKUKURU mkoa wa Njombe Bi,Domina Mukama ameyasema hayo wakati akitoa
taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo kwa kipindi cha
Januari-Machi 2020.
“Jumla
ya SACCOS na AMCOS 85 katika mkoa wa Njombe zilikuwa zinachunguzwa 14
Makambako,6 Ludewa,19 Makete,13 Wanging’ombe,35 hapa Njombe mjini zikidaiwa
jumla ya Tshs.7,965,449,650.04 ambapo kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Machi
2020 tumefanikiwa kuokoa kiasi cha Tshs. 1,769,161,693.31”alisema Mukama
Mukama
amesema hatua ni kutokana na agizo la Rais Dkt.John Pombe Joseph Magufuli alilolitoa ili kufuatilia
fedha za wananchi ambao ni wanachama wa vyama vya ushirika vya msingi AMCOS na
SACCOS ambazo zimeliwa au kufanyiwa ubadhirifu na viongozi wa taasisi hizo.
Aidha
amewapongeza wananchi wote waliojitokeza kulipa madeni hayo huku akiagiza
waliosali na ambao bado hawajajitokeza wajitokeze wenyewe kwa hiari yao.
0 Comments