TANGAZA NASI

header ads

Mrembo wa utalii Tanzania atua Njombe,waweka mkakati kutembelea vivutio



Na Amiri Kilagalila,Njombe

Wananchi mkoani Njombe  wameshauriwa kuenzi na kuvitembelea vivutio vya utalii vilivyopo ndani ya maeneo yanayowazunguka kwa lengo la kufahamu vyema rasilimali za taifa zilizopo Nyanda za Juu Kusini.

Rai hiyo imetolewa na mwakilishi wa mkoa wa Njombe katika shindano la mrembo wa utalii Tanzania, Zawadi Mwambi wakati alipotembelea ofisi za mkuu wa mkoa wa Njombe kwa ajili ya  kujitambulisha na kupata ushirikiano wa kuihamasisha jamii mkoani hapa na  kutumia wasaa wa kuvitembelea vivutio mbalimbali vilivyopo Nyanda za Juu Kusini ili kujifunza ..

"Leo nimefika katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Njombe kufanya mazungumzo ya kuangalia jinsi gani tunaweza kufanya ili kukuza vivutio vinavyopatikana katika mkoa wetu na kutoa elimu kwa jamii lakini zaidi mashuleni kwa wanafunzi waweze kutambua na kutembelea na wakipata elimu katika mashule naimani wataendelea kukua na ile elimu"alisema Zawadi Mwambi 

Baadhi ya wadau wa sekta ya utalii Nyanda za Juu Kusini akiwemo Michael Karam ameshauri kuwepo na hamasa ya serikali ya mkoa kuvumbua vivutio vipya vilivyopo..

"Ni lazima pia kuwepo utaratibu wa kuvumbua vivutio vipya ili wageni wa ndani na wa Nje waeze kuvijua na kuto kuvizoea vile walivyovizoea vya kila siku"alisema Michael Karam 

Naye Katibu  Msaidizi Uchumi na Uzalishaji katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Njombe, Ayoub Mndeme  amemshukuru mwakilishi wa mkoa wa Njombe katika mashindano ya urembo wa utalii na kuahidi mkoa kumpa ushirikiano katika kutangaza vivutio vya utalii mkoa wa Njombe.

"Kwa keli fursa za utalii zinahitaji kufahamika kuanzia kwa wanafunzi kama alivyozungumzia kwasababu haya ni maeneo ambayo sisi tupo na tunaishi na utalii imbao unahamasishwa sasa hivi ni ule wa ndani "alisema , Ayoub Mndeme  


Post a Comment

0 Comments