Na Amiri kilagalila,Njombe
Chama cha soka mkoa wa Njombe (NJOREFA) kimesema kinabariki maamuzi ya viongozi wa klabu ya Njombe Mji FC yakutangaza kutafuta wadau watakaoinunua timu hiyo ili iweze kuwa na ubora kuliko ilivyo sasa.
Katibu wa chama cha soka mkoa wa Njombe (Njorefa),Vicent Majiri amesema uamuzi huo unaweza kuwa na manufaa kwa klabu hiyo ambao tangu ianzishwe na kufanikiwa kucheza ligi kuu Tanzania bara msimu wa mwaka 2017/2018 kabla ya kushuka daraja haina ofisi ya klabu na kuachana na tabia ya kuwa ombaomba
"Tunaamini na wanachama nao wataendelea kuunga mkono wazo hili,lakini wazo la kihakikisha kwamba timu ya Njombe mji inakuwepo hilo ndilo la msingi,na uwepo kwa ubora sasa ni namna gani ndio hiyo ambayo inatafutwa lakini kuna Njia nyingine,akijitokeza kama mwanachama hivi hivi mimi ninayo pesa yangu hakuna haja ya kumuuzia mtu wala haina tatizo" alisema Majiri
Aidha katibu wa Njorefa amesema maagizo ya bodi ya ligi ya shirikisho la soka Tanzania (TFF) yanaitaka hadi ifikapo Juni 30, mwaka huu klabu ya Njombe iwe imepata ofisi kwa ajili ya kuiendesha klabu hiyo.
"Walikuja wakati timu ipo kwenye ligi kuu,sasa mpaka leo tumeendelea kuombaomba na tumeambaiwa mpaka mwezi wa saba tarehe 30 angalau hiyo ofisi iwepo" alisema tena Majiri
Kaini Nyigu ambaye ni msemaji wa klabu ya Njombe amesema hadi sasa hawajapata mnunuzi ingawa wapo walioonesha nia, huku changamoto zinazokabili timu hiyo kwa sasa ni pamoja na madeni ya mishahara ya wachezaji na benchi la ufundi.
"Hakuna mteja aliyejitokeza lakini kamati ya utendaji wanawaomba watu kadhaa ili waweze kuinunua"amesema Vicent Majiri
0 Comments