Na
Clief Mlelwa,Makambako
Waumini
wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania dayosisi ya kusini,wametakiwa
kuhakikisha wanavaa barakoa wanapofika ibadani.
Wito
huo umetolewa na askofu wa kanisa hilo dayosisi ya kusini Dkt,George Fihavango mara
baada ya ibada ya Jumapili katika kanisa la hilo usharika wa Mji Mwema mjini Makambako,ambapo
amesema kuwa waumini wote wanatakiwa kuvaa barakoa wanapokuwa ibadani ili
waweze kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona.
Aidha
ametoa wito kwa wakuu wa majimbo na wachungaji wa kanisa dayosisi ya kusini kuhakikisha
waumini wote wanavaa barakoa wanapokuwa ibadani.
Amesema
licha ya tahadhari ambazo zimeendelea kuchukuliwa na waumini wa madhehebu
mbalimbali katika kukabiliana na ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na
virusi vya corona (COVID-19) kwa kukaa umbali wa mita moja na nusu hadi mbili
na kunawa mikono kwa maji tiririka na sabun,lakini ni wajibu kila muumini
kufuata taratibu mbali mbali za kujikinga na virusi hivyo.
Amesema
waumini wote wanatakiwa kutambua kuwa kutokutii maelekezo yanayotolewa na
serikali ni kutokumtii Mungu,hivyo ni lazima wachukue tahadhali zote
zinazotolewa na wataalamu wa afya badala ya kumwomba Mungu pekee.
Naye
askofu msaidizi wa dayosisi hiyo Dkt Gabriel Nduye na kaim mkuu wa jimbo la Makambako
mchungaji Lyosi Mwalyosi wamesema utekelezaji wa agizo hilo la kila muumini
kuvaa barakoa linaanza mara moja kuanzia sasa na wamewataka waumini wote
kulipokea hilo kwa kulifanyia kazi kwa haraka.
Hata
hivyo baadhi ya waumini wa kanisa hilo,akiwemo Robart Bimbiga ,Rehema Goharimu
na Maria Gomano wamesema kuwa endapo washarika wote watavaa barakoa itasaidia
kwa kiasi kikubwa kukabiliana na virusi vya Corona.
0 Comments