Na Michael Patrick
Wanawake wamehimizwa kuwa mfano kulinda
watoto na watu wengine kuchukua tahadhari ya maambukizi ya virusi vya Corona.
Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa jumuiya
ya wanawake UWT mkoa wa Njombe,Rosemary Lwiva katika kikao maalum cha
kujadili taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM.
Mbele ya wajumbe wa umoja wa wanawake
UWT mkoa wa Njombe, mbunge wa viti maalum mkoa wa Njombe Dkt. Suzan Kolimba
amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM mkoa wa
Njombeo kwa kipindi cha miaka mitano, huku zaidi ya shilingi milioni mia tatu
na hamsini amesema zimetumika kuboresha miradi ya elimu, afya na ujasiriamali
katika halmashauri Sita za mkoa huo.
Katika kikao hicho, janga la Corona
limepewa kipaumbele ambapo wanawake wakiwa kama walezi wa jamii wamehimizwa
kutimiza wajibu wao kuzuia kuenea kwa maambukizi ya virusi vya Corona.
0 Comments