Mkuu wa wilya ya Njombe Ruth Msafiri akipimwa joto la mwili kabla ya kuingia kwenye kikao cha baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Njombe.
Wajumbe wa baraza la madiwani wakiwa katika kiko cha baraza kilichofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Mtwango
Afisa habari wa halmashauri ya wilaya ya Njombe Lukelo Mshaura akipimwa joto la mwili kabla ya kuingia kwenye kikao cha baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Njombe.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Ally Juma Ally akipimwa joto la mwili kabla ya kuingia kwenye kikao cha baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Njombe.
Katibu wa halmashauri ya wilaya ya Njombe Emanuel George akipimwa joto la mwili kabla ya kuingia kwenye kikao cha baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Njombe.
Na
Gabriel Kilamlya,Njombe
Halmashauri
ya wilaya ya Njombe imelazimika kuweka kipimo cha joto la mwili wa binadamu
kinachoitwa thermo scanner kwa ajili ya kuwapima wajumbe wanaokuwa wanashiriki
katika vikao mbalimbali ikiwa ni mkakati mojawapo wa kupambana na
maambukizi ya kirusi cha covid 19 kinachosababisha ugonjwa wa homa kali ya
mapafu.
Katika
kikao cha baraza la madiwani cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha wa 2020/2021
mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Njombe Valentino Hongoli amesema
kuwa ni lazima mapambano ya virusi vya corona yaendelee kwa kutoa elimu
kwa wananchi juu ya kujikinga na ugonjwa huo.
Akitoa
salaam za serikali mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri amewataka wataalam wa
afya kuwasimamia wajasiriamali wanaofanyakazi ya kushona barokoa za vitambaa
kuhakikisha wanashona zenye ubora unaotakiwa huku akishauri halmashauri
kuvitumia vikundi vilivyopo na vinavyonufaika na mikopo ndani ya halmashauri
hiyo kujishonea barakoa zao ambazo zinaweza kuuzwa hata nje ya halmashauri.
Veronica
Maganga ni mtaalam wa maabara katika kituo cha kutolea huduma za afya cha Mtwango
ambaye amekuwa akiwapima joto washiriki wa vikao na madiwani wakati
wakiingia kwenye kikao anasema kuwa kipimo hicho kinachosoma kuanzia joto
la sentigradi 34 kwenda juu kinasaidia kutambua joto linalotakiwa katika mwili
wa binadamu na kubaini dalili moja wapo ya maradhi katika mwili wa
binadamu.
Kwa
upande wake mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Njombe dokta Deusdedit Kalaso
upimaji huo ni ni mkakati wa kuhakikisha wanaendelea kukabiliana na virusi
vya Corona.
Bado
mapambano dhidi ya ugonjwa wa corona yanaendelea nchini kote huku jamii
ikitakiwa kuendelea kuzingatia kanuni za wizara ya afya ikiwemo kunawa
mikono kwa sabuni na maji tiririka.
0 Comments